Join us on facebook page

Thursday, 19 December 2013

HIZI NDIO HABARI NJEMA KUHUSU TOZO YA KODI KWA LINE ZA SIMU KUTOKA KWA JANUARY MAKAMBA

Habari za kodi kwa laini za simu ilichukua vichwa vya habari kwa wakati wake hadi pale mheshimiwa Rais alivyotoa agizo kwa wahusika kulishughulikia hili suala.
Naibu Waziri mwenye dhamana ya mawasiliano,sayansi na teknolojia “January Makamba” ametoa habari mpya na nzuri  kuhusu kodi hii.
Kupita ukurasa wake wa facebook alipost “Mheshimiwa Rais ametia sahihi Hati ya Dharura (Certificate of Emergency) kufanyika marekebisho kwa Muswada wa Fedha wa mwaka 2013 kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu (SimCard Tax). Asante Mheshimiwa Rais.”.
Read more ...

SAMWELI ETOO AAMBULIA MATUSI YA NGUONI KUTOKA KWA MASHABIKI WA CHELSEA BAADA YA KUPOST TWEET HIIMashabiki wa Chelsea wanamrushia matusi pamoja na maneno ya kebehi striker Samuel Eto’0 baada ya kupost picha ambayo sio kawaida kwa mchezaji ku-tweet pale timu yake inapokua imepata matokeo mabaya uwanjani.
Picha yenyewe ni hii hapa chini inaonyesha matokeo ya Chelsea dhidi ya Sunderland then Samuel Eto’o aka-tweet kwa followers wake zaidi ya laki moja na nusu kitu ambacho baadhi yao wamekichukulia vibaya kwamba kwa nini timu ifungwe alafu apost?
etoo
Hizi ni baadhi ya tweets kutoka kwa mashabiki ambapo tweet nyingine zina maneno mazito kutoka kwa mashabiki hawa ambao wamemjibu Samuel.e1
e2
e3
e4

Read more ...

DR SLAA TUKISHIKA DOLA TUTARUHUSU UTENGENEZAJI WA POMBE YA GONGO KISHERIA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.
Read more ...

BABY MADAHA: DIAMOND HANIWEZI, AWATISHIE WATOTO TANDALE

MWIGIZAJI na mwanamuziki Bongo, Baby Joseph Madaha amemchana Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kumwambia awatishie watoto wa Tandale kwani hana ubavu wa kuchuana naye.

Akizungumza na paparazi wetu, Baby alifunguka kuwa anamshangaa Diamond kujibu kuhusu jinsi alivyomchana wiki kadhaa zilizopita gazetini na kusema yeye hamuwezi kwani alimtangulia kuchomoka kistaa.

“….akiwa bado ana-struggle kupata mkwanja awatishie watoto wenzake wa Tandale, mimi nishazindua brand yangu ya manukato na mikoba ya zawadi, bidhaa ambazo zinaingia sokoni rasmi Desemba 31, awatishe haohao watoto wenzake, mimi siyo saizi yake,” alisema Baby. 
Diamond alipotafutwa, simu yake iliita bila kupokelewa.
Read more ...

JACK WOLPER NA ZAMARADI NDANI YA BIFU ZITO

Na Shakoor Jongo
STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema kuwa ni mnafki na adui yake mkubwa katika maisha.

Akizungumza na Amani juzikati, Wolper alisema amegundua kuwa mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana maisha yake kwa mtindo wa chanya (negative), akamuomba amuache.

“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.

“Huko nyuma kupitia kipindi chake alikubali nidhalilishwe na waigizaji wenzangu kwa faida yake (hakutaka kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi karibuni)  kaniweka hewani (kwenye redio) bila ya ridhaa yangu. Naomba niseme kuwa naanza kugundua azma yake kwangu ni nini, aniache na maisha yangu,” alilalama Wolper.

Baada ya Wolper kulalamika sana, Amani lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.

“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.
GPL

Read more ...

RAY C AANIKA VIGEZO VYA MUMEWE MTARAJIWA

Na Gladness Mallya
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kusema kuwa anahitaji mume anayemzidi umri kwa miaka kumi.

Akizungumza hivi karibuni kwenye kituo kimoja maarufu cha runinga, Ray C alisema anahitaji mwanaume mtu mzima anayemzidi miaka kumi, anayejitambua na asiwe mwanamuziki kwani anaamini akiwa na mtu kama huyo uhusiano wao utakuwa mzuri kuliko ule wa awali uliokuwa wa machungu.

“Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka 31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu.

“Nashukuru sasa hivi niko vizuri nakumbuka  meneja wangu wa kwanza alinikataza nisiwe na uhusiano na mwanamuziki lakini ndiyo hivyo nikajikuta niko na Lord Eyes ambaye alianza kunichanganyia cha Arusha (bangi) bila mimi kujua na kujikuta ninaharibikiwa lakini nimeshamsamehe na ninamuombea heri katika maisha yake,” alisema Ray C.

Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana kwa mwanaye.

“Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C.

Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa maisha yake.

Read more ...

LULU: KAMA SI KANUMBA YANGENIKUTA MAZITO


SURA ya mauzo katika sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ametoa ya moyoni kuwa kama siyo kuwekwa nyuma ya nondo za Mahabusu ya Segerea, Dar basi yangemkuta mazito.

Lulu alikaa Gereza la Segerea kwa takribani miezi kumi baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.
Nyota huyo wa Filamu ya Foolish Age alifunguka mambo ya kushangaza hivi karibuni juu ya tukio hilo kupitia Kipindi cha Take-One, kinachorushwa  na Clouds TV.

TATIZO FOOLISH AGE
Lulu alikuwa akizungumzia filamu yake hiyo ya Foolish Age ambapo alisema sinema hiyo inawasihi wasichana ambao wanapitia kipindi cha balehe ambacho ni hatari sana kwao.
“Kwa kweli kipindi cha foolish age ni cha hatari sana, nilicheza filamu hiyo ili kuwaasa wasichana wenzangu.
“Asikwambie mtu, mimi mwenyewe nilikokuwa nikielekea si kuzuri kabisa.

KAMA SIYO KANUMBA
“Ukweli ni kwamba kama siyo matatizo (kifo cha Kanumba) nikaenda mahabusu sijui ingekuwaje sasa hivi. Kukaa jela kulinisaidia kusitisha kasi ya tabia yangu, nikatoka nikiwa mpya.
“Yangenikuta mazito zaidi maana kipindi kile ilikuwa hatari tupu,” alisema Lulu ambaye ni mrembo wa haja.

Staa huyo aliongeza kuwa kipindi hicho kilikuwa cha hatari na hakitamani kijirudie hata kidogo katika maisha yake.
Alisema kwamba si ajabu inawezekana kipindi hicho ndicho kilisababisha matatizo yote yaliyomkuta. Alisema alikuwa akielekea kubaya.

HATAKI KIJIRUDIE
“Ni kipindi ambacho siwezi kukuhitaji tena katika maisha yangu si kizuri na kinatisha maana kuna wakati nilikuwa sisikii la mtu yeyote hata mama yangu mzazi,” alisema Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu haonekani akirandaranda mjini kama zamani.
Kabla ya utulivu huo alioupata nyuma ya nondo, Lulu alikuwa hakauki kwenye kumbi za usiku za starehe huku akilewa tilalila na kuyaweka maisha yake hatarini endapo angefanyiwa kitu mbaya.

Lulu alihusishwa na kifo cha Kanumba kwa kuwa siku ya tukio alidaiwa kuwa naye eneo la tukio ambapo alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana akisubiri kesi ya kuua bila kukusudia.


SKENDO MPYA
Wakati hayo hayajapoa kumeibuka skendo mpya inayomgusa staa huyo mkubwa Bongo.
Madai mazito yameshushwa na wafuatiliaji wa mambo ya watu kuwa nyuma ya mwanadada huyo anayeng’ara kuna mbunge maarufu anayemiliki jimbo kwa kura za wananchi jijini Dar (tutamtaja baadaye).

ILIKUWA HIVI
Sosi: Hivi ninyi Global siku hizi hamuandiki skendo za mastaa?
Global: Tunaandika sana kwani vipi?
Sosi: Mna habari?
Global: Tunazo nyingi fuatilia magazeti yetu lakini ukitupatia ya kwako tutairusha hewani.
Sosi: Sasa mimi nina habari yangu.

Global: Inakuhusu wewe? Funguka. 
Sosi: Hainihusu mimi. Ni ya ‘Kalulu Kadogo’.
Global: Siku hizi amekua, sema Lulu inatosha. Eeh... hiyo habari ikoje?
Sosi: Kwa taarifa yenu siku hizi anatoka na mbunge (anamtaja). Ndiye kamnunulia lile gari analokatiza nalo mjini na kampangishia bonge la mjengo kule Tegeta (Dar). Fuatilieni kwa watu wake wa karibu, naombeni msinitaje.
Global: Hatuwezi kukutaja ngoja tuzame mzigoni.

Gazeti hili lilifanya uchunguzi wake kwa watu wa karibu wa Lulu na kubaini kuwa ni kweli kwa sasa staa huyo amehama Tabata alikokuwa akiishi na mama yake, Lucresia Karugila na kuhamia kwenye bonge la mjengo Tegeta huku akisukuma gari kali (aina haikujulikana mara moja).
Madai mengine yalisema kwamba  mke wa mbunge huyo alishamtafuta Lulu na kumuonya kuachana na mume wake


LULU AFYATUKA  
Baada ya kujiridhisha kuwepo madai hayo, juzi gazeti hili lilimtafuta Lulu na kumsomea mashitaka yake mwanzo hadi mwisho ambapo alifyatuka:
“Hivi ni nani anayeleta habari zangu Global? Analipwa na nani? Maana kila kukicha unasikia hili, halijapoa unasikia lingine.

“Si kweli kwamba natembea na huyo mbunge. Kwanza sina mazoea naye. Nakumbuka nilimuona mara moja tu sikumbuki ilikuwa kwenye shughuli gani.
“Huyo mkewe mimi simjui anafananaje. Nasema huko ni kuchafuana kusikokuwa na maana.”

VIPI KUHUSU KUPANGISHIWA NYUMBA?
“Ni kweli nimehamia Tegeta lakini sijapangishiwa, nimepanga mwenyewe. Hivi nikifanya jambo lazima iwe kuna mwanaume? Watu waache hizo. Wabadilike.”

VIPI KUHUSU GARI?
“Gari ninalo muda mrefu nimenunua kwa fedha yangu. Halina mkono wa mbunge, ni jasho langu.”
Kabla ya kuwekwa mahabusu, Lulu aliwahi kudaiwa kuhongwa nyumba na mbunge mwenye kitambi kikubwa, ishu hiyo aliikanusha kwa nguvu zote.

Imeandikwa na Imelda Mtema na Musa Mateja.
Gpl

Read more ...